23 Machi 2025 - 17:00
Asilimia 30 ya ongezeko la idadi ya Mazuwwari kwenye Madhabahu (Haram) ya Imam Ali (AS) katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Idadi ya Mazuwwari wa Madhabahu ya Imam Ali (AS) iliweka rekodi katika siku ya 21 ya Ramadhani, na mwaka huu, mahujaji milioni moja na 500,000 zaidi wametembelea (wamezuru) Madhabahu ya Alawi kuliko mwaka jana.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s.) - Abna -;  "Watu milioni 6, 391 elfu na 390 wametembelea Kaburi (Haram) Tukufu la Imam Ali (amani iwe juu yake) wakati sambamba na kumbukumbu ya Kifo chake cha Kishahidi"; Habari hii ilitangazwa na Haram ya Alawi (a.s).

Mwaka jana, katika siku kama hii, Haram ya Alawi (a.s) ilikuwa na Mazuwwari wasiozidi milioni 5, na mwaka huu, takriban watu milioni 1.5 zaidi wameongeza katika kutembelea Haram Tukufu ya Alawi kuliko ilivyokuwa kwa mwaka jana.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha